Vanessa Mdee Aamua Kuonyesha Mashabiki Wake Cover ya Albamu

Vanessa Mdee Aamua Kuonyesha Mashabiki Wake Cover ya Albamu
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, Msanii Vanessa Mdee ameamua kuwaonesha mashabiki wake cover ya Albamu yake ambayo anatarajia kuitoa na hii ikiwa ni albamu yake ya kwanza tangu aingie katika gemu la muziki wa Bongo fleva.


Hapo nyuma, Vanessa Mdee aliwaahidi mashabiki zake kuwa , kabla ya mwaka huu 2017 kuisha, atatoa Albamu yake yenye nyimbo18 ambayo itakuwa imewashirikisha wasanii wa Tanzania na nje ya Tanzania.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Vanessa Mdee ameonyesha kava ya albamu hiyo (Muonekano) na kuthibitisha hiyo ndio yenyewe kwa kuandika,


"This is the official album cover #MoneyMondaysTheAlbum".

Tusubiri tarehe rasmi ya albamu hiyo na kuweza kuwafahamu zaidi watu aliowashirikisha katika Albamu hiyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad