Wafanyabiashara Wafunguka Ugumu wa Biashara Msimu Huu wa Sikukuu

Wafanyabiashara Wafunguka Ugumu wa Biashara Msimu Huu wa Sikukuu
Leo ni sikukuu ya Krismas ambayo huadhimishwa na Wakristo duniani kote kila ifikapo Disemba 25 kila mwaka, ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kwa upande wa biashara mambo yamekuwa tofauti, wafanyabiashara wamelia hali kuwa ngumu.


Wafanyabiashara katika Soko la Mwenge wameeleza kuwepo kwa ugumu katika biashara zao wakilalamikia ugumu wa biashara na upatikanaji wa wateja katika sikukuu hizi za mwisho wa mwaka.

Akiongea na kipindi cha Supa Mix cha East Africa Radio leo, mfanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Mwenge jijini Dar es Salaam Dokta J Pamba, amesema hali ya biashara sio nzuri kwa mwaka huu.

“Hali ni mbaya kibiashara, zamani msimu wa sikukuu watu walikuwa wanakuja na familia zao lakini saivi anakuja mmoja mmoja, watoto wanakuwa nyumbani na mauzo yanakuwa kidogo kwasababu wananunua nguo moja, kiujumla biashara ni ngumu”, amesema Dokta J.

Kwa upande wa wateja waliozungumza na Supa Mix wamesema bei za bidhaa ziko juu na wamekiri kuwepo kwa upandishwaji wa bei katika kipindi hiki cha sikukuu lakini wamedai haiwazuii kufanya manunuzi kutokana na uhitaji walionao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad