Wanahabari Wajitosa Ishu ya Lissu, Ben Saanane, Azory Wambana DCI

Wanahabari Wajitosa  Ishu ya Tundu Lissu, Ben Saanane, Azory Wambana DCI
MKURUGENZI wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, amesema kuwa matukio ya kihalifu kwa mwaka huu wa 2017, yamepungua sana ambapo ameeleza kuwa kutokana na takwimu inayoonyesha kwamba mwaka jana 2016, matukio yaliyoripotiwa ni 68, 204 ikilinganishwa na matukio 61, 774 ya mwaka huu.

Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari DCI Boaz, aliulizwa kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kupotea kwa mwandishi wa Azory Gwanda pamoja na tukio la kupotea kwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Ben Saanane, iwapo hatua za kiuchunguzi kubaini waliotenda makosa hayo na taarifa za awali kuhusiana na kupotea kwa watu hao zimefikia wapi.

DCI Boaz, kuhusu tukio la kupotea kwa mwandishi Azory amesema kuwa wanachukua kila hatua, na kuwaomba wananchi wawe na subira wakati jeshi linaendelea kuchukua taratibu zinazotakiwa.

Kuhusu Ben Saanane, Boaz amesema kwa mujibu wa kanuni za kiupelelezi taarifa hazitakiwi kuwekwa hadharani, na pia amwaomba wananchi kwa yeyote ambaye ana taarifa ambayo itawasaidia katika upelelezi wao, basi aiwasilishe wao wataifanyia kazi.

Aidha kuhusu Tundu Lissu, amesema jeshi la polisi inaendelea na uchunguzi na kwamba wanachukulia tukio hilo kwa umakini zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad