Wananchi Wampa Makavu Maulid Mtulia Baada ya Kutangaza Kugombea Ubunge Kupitia CCM Baada ya Kuikimbia CUF

Aliyekuwa Mbunge Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho  tawala.

Desemba 2 Mtulia alijiuzulu nafasi ya ubunge,  huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.

Baada ya hatua hiyo, chama cha CUF upande wa Profesa  Ibrahim Lipumba  kilitangaza  kuwaomba radhi wapiga kura wa Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha ubunge.

Lakini  jana Jumanne Desemba 19, 2017 kupitia andiko lake mtandaoni, Mtulia amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa  ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena nafasi hiyo.

"Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu" aliandika Mtulia

Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza nia yake kutaka kugombea; "Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni"

Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi ya wananchi walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya na analotaka kulifanya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad