Wananchi wa kijiji cha Msosa kilichopo Kata na Tarafa ya Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo mkoani Iringa wameiondoa kamati ya Mipango na Fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za kijiji.
Uamzi huo umefikiwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo na baada ya kuwaondoa viongozi hao wanakijiji waliunda kamati mpya kwaajili ya kusimamia majukumu hayo.
Kwa upande wake mtendaji wa Kata hiyo Maiko Chabila ameafiki kuvuliwa madaraka kwa viongozi wa kamati ya mipango na fedha kutokana na tuhuma zinazowakabili.
East Africa Television imemtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah, amesema suala hilo bado halijafika ofisini kwake lakinitayari ameshatuma wawakilishi wake kuhakikisha wanalifuatilia na kupata ufumbuzi wake.
Hata hivyo kamati hiyo ya Mipango na Fedha ya kijiji cha Msosa wamekubali kujiudhuru pamoja na kulipa pesa ambazo zimebainika kuwa walizitumia vibaya bila kuwashirikisha wananchi.