Wanaume Watakiwa Kuhudhuria Kliniki na Weza Wao

Wanaume Watakiwa  Kuhudhuria  Kliniki na  Weza Wao
Afisa Muuguzi msaidizi katika Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Shinyanga, Dk. Rehema Kapita, ametoa wito kwa wanaume kujenga tabia ya kuhudhuria kliniki na wenzi wao pale wanapokuwa wajawazito, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.


Amesema idadi kubwa ya wanaume mkoani Shinyanga hawana utamaduni wa kuhudhuria kliniki na wenzi wao, hivyo kukosa elimu ya afya ya uzazi tangu malezi ya mimba hadi kujifungua, na kupelekea mzazi kukosa huduma stahiki
za matunzo na kusababisha kujifungua kwa shida ama kupoteza maisha .

Ametoa wito huo jana wakati akizungumza na Nipashe katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga, kuzungumzia watoto waliozaliwa kwenye mkesha wa sikukuu ya Kristimas ambapo watoto 14 walizaliwa wakiume wa tano, tisa wa kike na wote wakiwa salama.

“Natoa wito kwa kinababa kujenga utamaduni wa kuhudhuria kliniki na wenzi wao ili wapate elimu ya afya ya uzazi, pamoja na malezi ya mimba hadi kujifungua kwa lengo la kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi, sababu watashirikiana kwa pamoja namna ya kumtunza mtoto na hatimaye mama kujifungua salama,” amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad