Wapinzani Wameshapotezana – Wakili Msomi ‘Alberto Msando’

Aliyewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo na Wakili msomi wa kujitegemea, Alberto Msando amesema vyama vya upinzani nchini vimekosa nguvu katika kupambana na rushwa ukilinganisha na chama tawala cha CCM.

Msando amesema hayo leo tarehe 10 Desemba 2017, mjini Dodoma kwenye mkutano mkuu wa UVCCM taifa uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli.

“Wapinzani siyo tu wanapotezana, bali hadi sasa wameshapotezana, tumeshawapiga 4-0 ugenini na tukirudi nyumbani nako ni 4-0, tunamaliza kazi, CCM Oyee!!” – Alberto Msando

Alberto Msando ni moja ya watu mashuhuri saba waliohamia CCM kutoka kwenye vyama vya upinzani.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe ndo umepotea. Hujielewi. Adabu za ukondoo. Hazina tija. Hivi hujielewi. Mlikuwa shujaa na kundi. Umerudi kulekiule. Kwenye wengi wenye vitambi na mabwenyenye.

    ReplyDelete
  2. Karibu sana Msando. Umerudi Nyumbani na Tunakuhitaji katika Kuendeleza Chama na Nchi Kwa Ujumla.
    Hatua uliyo chukua ni Stahiki katika Wakati Stahiki Nchi inakuhutajini nyinyi Vijana Kusukuma Chama Chetu Na Nchi yetu.

    Wenye Wivu na Madonge Wajinyonge... Na chuki zao hazina kasi wala Tija.
    Watakuoneni hivi hivi na watasema sana. CCM Oyeeeeeeeeee. Msando Oyeeeeeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad