Watoto Sita wa Mwaka Mmoja Wapelekwa Israel kwa Ajili ya Matibabu ya Moyo

Watoto Sita wa Mwaka Mmoja Wapelekwa Israel kwa Ajili ya Matibabu ya Moyo
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka  watoto sita wenye umri wa mwaka mmoja hadi  13  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari hiyo wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana. Baada ya matibabu kukamilika  wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano JKCI imeeleza licha ya Taasisi hiyo kutoa matibabu pia ina mkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Hili ni kundi la tano la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad