Waziri Aagiza Wafanyakazi Kuongezewa Malipo

Waziri Aagiza Wafanyakazi Kuongezewa Malipo
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Dkt Omari Mponda, kuwaongeza malipo ya kazi wafanyakazi wa kituo hicho katika mradi wa kubangua Korosho.


Naibu waziri Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipotembelea kiwanda kidogo cha kubangua Korosho na kubaini wafanyakazi wanalipwa shilingi 600 kwa kila kilo moja ya korosho wanayobangua kiasi ambacho hakiakisi ufanisi wa kazi kubwa wanayoifanya.

Katika maelekezo yake Naibu Waziri huyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho kuongeza kiasi cha malipo walau kufikia shilingi 1000 kwa kila kilo moja ili wafanyakazi hao waweze kupata malipo ambayo yatamudu gharama za maisha.

Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa/kugundua na kusajili mbegu bora 54 za korosho kwa ajili ya matumizi kwa wakulima mwaka 2006 (Aina 16), Mwaka 2015 (Aina 22 mbegu chotara), na Mwaka 2016 (Aina 16 mbegu fupi).

Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele (NARI) imepewa jukumu la kufanya Utafiti ili kuongeza tija katika Kilimo katika kanda ya kusini mikoa ya Lindi, Mtwara na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad