Waziri wa afya wa Zanzibar Mahmud Thabit kombo amesema asilimia 33 ya jamii ya Zanzibar inaviashiria vya ugonjwa wa figo huku akisitiza kuwa sera ya serikali kutoa huduma bila malipo iko pale pale na tayari wagonjwa wa figo na magonjwa mengine wanapata huduma hizo bila malipo.
Akizungumza na wandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa madawa kutoka kwa ubalozi mdogo wa Oman hapa Zanzibar Mhe Mahmud amesema ugonjwa huo ni tishio na serikali imelazimika kuhakikisha ina mashine za kusafisha figo .
Naye Mkuruegnzi wa kinga na elimu ya afya Dr Fadhil Abdullah amesema utafiti uliofanywa hadi sasa unaonyesha ugonjwa huo wa figo unawagusa asilimia 33 ya jamii na hii inatokana na wagonjwa wengi wa shinikizo la damu na sukari kuongezeka Zanzibar ambayo ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa huo,huku balozi mdogo wa Oman Dr Ahmed Hamood Al Habshi ambaye alikabidhi dawa hizo amesema serikali yao Oman iko tayari kusiaiida Zanzibar katika kupamabana na ugonjwa huo na mengine kwa kutoa utaalamu na vifaa.
Wizara ya afya kupitia vitengo mbali mbali vikiwemo vya saratani,sukari na magonjwa yasiyoambukiza vimekuwa vikitoa elimu ya afya kwa wakazi wa Zanzibar wabadilike katika ulaji wa vyakula na kuanza kufanaya mazoezi kutokana na ongezeko la magonjwa hayo.