Waziri Kalemani Chadema Wabanwa Koo

Waziri Kalemani Chadema Wabanwa Koo
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amewaagiza Mameneja wote wa Shirika la Umeme nchini, Tanesco, kuhakikisha wananchi wote ambao wamelipia gharama za kuunganishiwa umeme wanafanyiwa hivyo kabla ya mwaka huu haujamalizika .


Dk. Kalemani ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muungano Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, kuhusu mpango wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini, REA ambapo kijiji cha Muungano ni miongoni mwa vijiji 33 vitakavyounganishiwa nishati hiyo.

Amesema kuanzia sasa mteja ambaye tayari amelipia gharama za kuunganishiwa umeme, Tanesco inapaswa kumuunganishia umeme ndani ya siku saba na wale ambao wamelipia ndani ya mwaka huu wanatakiwa waunganishiwe umeme kabla ya mwaka huu haujaisha.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, amesema, umeme katika baadhi ya vijiji vya jimbo lake kikiwemo kijiji cha Muungano ni shida hivyo kuomba awamu hii ya tatu ya mradi wa REA kuwaanganishia na kuwawekea Transfoma yenye uwezo mkubwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad