Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam ambapo alibaini uwepo wa makontena yenye magogo ambayo ni mazao ya misitu yaliyokaa bandarini hapo kwa zaidi ya miaka 10.
Waziri Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo hayo 938 na kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali.
Aidha Dkt. Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka nchini Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia na yalivunwa wapi na kwa vibali gani vya nchi hiyo pamoja na kufuatilia nyaraka za kuingiza ndani ya Tanzania.
Ameagiza kitengo cha kuzuia ujangili kifuatilie kubaini uhalisia na uhalali wa taarifa hizo vinginevyo yatakuwa mali ya Serikali.
Dkt. Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika, pia uwepo wa taarifa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanaotoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria, hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu yetu ya asili.
Hahaa..picha linazidi kuboa... haya, aende wa nne, nae aibue vyake.
ReplyDeleteSerikali ya Magufuri iko kazini, inatekeleza Ilani ya hapa Kazi, Tanzania mpya hiyo, manakee hata dunia inatuelewa Sasa. Na ukichukulia kuna usemi wanasema kamba watu weusi ni wavivu sana wa kufanya kazi mpka kufikiria ni wavivu, Lakini si kwa serikali ya Baba Magu ni wachapa kazi na wepesi wa kufikiria wafanye Nini. Kuiweka nchi yao iende sawa,
ReplyDeleteBandarini ni Lazima kuwa na CCTV kila pembe na monitored Central police na PCCB na TRA na TPA.
ReplyDeleteWaliona kisicho eleweka au kutilia shaka ni Papo hapo. Unawawajibisha wale makamishna waliokuwepo katika ulingo wa Bandari.
Magu kwa Spidi hii anaiweza nchi na Watanyooka Tu.
Hongera Watanzania Kutuchagulia JEMBE. Hili Si Buldozer la Kawaida... Hili ni D8+D12 Mbele kwa mbele Hataki mchezo...... Hapa Kazi Tuuuuuuuuuuu. na Uaminifu