WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kuaga miili ya askari 14 waliouawa na waasi wa ADF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo shughuli ya kuaga miili ya askari hao imefanyika leo Alhamisi, Desemba 14, 2017 katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine waliohudhuria katika kuaga miili hiyo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, wakuu komandi za anga, maji, nchi kavu na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), viongozi wa Umoja wa Mataifa, na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari na wananchi.
Baada kukamilika shughuli ya kuaga miili hiyo itasafirishwa kwao mazishi.
Waziri Mkuu Aongoza Waombolezaji Kuaga Miili ya Askari 14 wa JWTZ Waliouwawa na Waasi DRC
0
December 14, 2017
Tags