Waziri Mkuu wa Uingereza Amfukuza Kazi Naibu Wake

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amefukuza kazi Naibu wake, Damian Green baada ya kugundulika alidanganya kuhusu kwa video za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya bungeni

Uchunguzi kwenye ofisi ya baraza la mawaziri ulisema alitoa taarifa ambazo sio sahihi na za kupotosha akikataa kuwa alijua kuhusu kugundulika kwa video hizo kwenye uvamizi wa polisi kwenye ofisi za bunge mwaka 2008

Green alilazimishwa kujiuzulu baada ya washauri kwenye masuala ya mawaziri kusema alivunja maadili ya uwaziri

Green alikuwa mshirika mkubwa wa waziri mkuu, na kuondoka kwake kutakuwa ni pigo kubwa kipindi hiki ambacho Uingereza inapitia kwenye majadiliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad