Waziri Mwakyembe Achimba Mkwara ‘Mazoea’ Taifa Stars

Waziri mwenye dhamana ya michezo Tanzania Dr. Harrison Mwakyembe amesema suala la uwakilishi kwenye timu ya Taifa kwa mazoea inabidi liangaliwe kwa makini kwa sababu kuna wachezaji wamekuwa na uhakika wa kuitwa kwenye timu hata kama hawajitumi wakiwa kwenye timu hiyo.

Waziri Mwakyembe amesema hata yeye ameumizwa na matokeo yaKilimanjaro Stars kwenye Challenge Cup kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu ambapo timu hiyo haikushinda hata mechi moja kati ya nne ilizocheza hatua ya makundi huku ikitupwa nje ya mashindano ikiwa na pointi moja iliyoipata baada ya suluhu dhidi ya Libya kwenye mechi ya kwanza.

“Sasa uwakilishi kwenye Taifa Stars kwa mazoea hili suala lazima tuliangalie kwa makini sana. Sio mchezaji anakuwa anauhakika wa kuitwa kwenye timu, tunataka tuone kwa kujituma”-Mwakyembe.

Mwakyembe pia amesema kutokana na wachezaji wa Zanzibar Heroes wanavyojituma kwenye michuano ya Challenge Cup 2017, anaamini watarudi na kombe hilo.

“Kwa mchezo wanaouonesha vijana wa Zanzibar Heroes nina uhakika hili kombe tunalipata, litakuja Tanzania. Wanacheza kwa kujituma, sio mtu anacheza kwa kujituma nusu kwa sababu atajituma zaidi akiwa kwenye klabu, nafiri nimejifunza vizuri sana kama Waziri katika sekta hii.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kweil utaona jinsi gani vijana wetu walivyokuwa hawana malengo na kazi wanayoifanya. Wachezaji wengi wa Kilimanjaro stars wanatokea aiza club bingwa wa Tanzania au mshindi wa pili au mshindi wa watu. Ni club ambazo pia ndizo zitakazowakilisha nchi katika mashindano ya vilabu kwa ngazi ya kimataifa. Kwa hivyo hapana shaka yeyote mashindano yale ya challenge cup ni moja kati ya sehemu ambayo wanakuwepo mascauti au mawakala wa kutafuta na kufuatilia nyendo na uwezo wa mchezaji kwa ajili ya kuwanunua. Zile ni sehemu hadimu za mchezaji kuonesha uwezo wake si kwa ajili ya kulipigania Taifa tu peke yake bali kujipigania wao wenyewe binafsi kwa kuonesha uwezo wao duniani kujitangaza. Inaonekana wachezaji wa kizanzibari wameelimishwa na kulielewa suala hili vizuri na wanapaswa kupongezwa sana. Sasa ikiwa wachezaji hawa hawa wa Kilimanjaro stars ndio wachezaji wa simba na yanga kweli kuna mtanzania anaewaza vilabu hivi kufanya vizuri Africa? Bahati nzuri hivi vilabu vina wachezaji wa kigeni labda hawa watakuwa na malengo ya mbali na moyo tofauti wa kujitoa kwa ajili ya kazi zao. Tatizo jengine ni makocha kwa kipindi kirefu sasa hakujapatikana kocha mwenye uwezo wa kusimamia timu zetu kushindana kimataifa. Mfano ni sawa ya kumuandaa mnyanyuwa vyuma kwa kumfanyisha mazoezi ya kunyanyua chuma cha kilo 30kg wakati kwenye mashindano anakwenda kunyanyua chuma cha kilo 100kg. Tunahitaji makocha wenye uwezo wa kuwaandaa wachezaji wetu ili kupata ushindi zidi ya timu zenye uwezo Africa lakini bila ya hivyo tutakuwa washindikizaji mpaka Dunia inakwisha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad