Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa.
Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bwana Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018