Zambia Yasitisha Ajira ya Polisi wa Kichina

Zambia Yasitisha Ajira ya Polisi wa Kichina
Maafisa wa polisi nchini Zambia wamefutilia mbali mpango wa kuwaajiri raia wanane wa Kichina kuwa polisi nchini humo yapata saa 24 baada ya kuzindua mpango huo kufuatia pingamizi kutoka kwa raia.

Maafisa hao wapya walikuwa wamepewa jukumu la kupiga doria mjini Lusaka siku ya Jumatatu.

Lakini uamuzi huo ulizua hisia kali kutoka kwa raia hususan kutokana na agizo jipya lililotolewa mapema mwaka huu ambalo linapiga marufuku maafisa wa polisi kuoa wageni kutokana na sababu za kiusalama.

Raia wa Zambia wenye uraia wa mataifa mawili pia hawaruhusiwi kujiunga na kikosi cha polisi.

Nyani azima umeme kwa karibu masaa 6 nchini Zambia
Kenneth Kaunda atimiza miaka 93
Dickson Jere, ambaye ni wakili, alisema kuwa uteuzi huo ulikiuka katiba ambayo inasema wazi kuwa, Mzambia yeyote aliye na uraia wa nchi mbili hawezi kujiunga na idara za usalama.

Msemaji wa polisi nchini Zambia Esther Mwata-Katongo, alitetea uteuzi huo wa polisi akisema kuwa kabla ya wao kuteuliwa walichunguzwa na watafanya kazi chini ya usimamizi wa polisi wa kawaida.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad