“Z’bar Wakipewa Uanachama CAF na FIFA wanafuzu AFCON na World Cup”-Zitto

Mara tu baada ya timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ kuichapa Uganda kwa bao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Chalenji na kutinga fainali ya michuano hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye account yake ya facebook.

Zitto ni mdau mkubwa wa michezo hususan soka amesema ikiwa Zanzibar itapewa uanachama wa CAF na FIFA ndani ya miaka mitano, itafuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) na hata fainali za kombe la Dunia.

“Zanzibar Heroes wanatutoa kimasomaso huko Kenya jamani. Ni lazima sasa tupambane Zanzibar iwe na uanachama FIFA kama Zanzibar.”

“Kama hatutaki Zanzibar kuwa Mwanachama wa FIFA kama ilivyo Scotland. Tuseme kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu ZFA ndio mwanachama FIFA na CAF ili TFF ipate muda wa kujipanga. Ndani ya hiyo miaka 5 nawaambia Zanzibar itakwenda AFCON na hata Kombe la Dunia. #MsemaKweliMpenziWaMungu”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mh*#** we Zito Kabwe ni shida tu kila kitu kwako ni siasa. Hakuna timu kwenye ukanda huu wa Africa mashariki yenye nidhamu na jitihada kama Uganda hata kule kenya wamepeleka kikosi cha pili lakini bado wanahangaikia ticket ya kwenda kushiriki fainali za Afcon achilia mbali kombe la Dunia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad