Zitto Aingilia Kati Sakata la Airtel, TTCL Ataka Ukaguzi Maalumu Ufanyike

Zitto Aingilia Kati Sakata la Airtel, TTCL Ataka Ukaguzi Maalumu Ufanyike
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameshauri kutazamwa mchakato mzima wa ubinafsishaji kwa kufanya ukaguzi maalumu wa sera ili kutoa mapendekezo ya kurekebisha makosa yaliyofanyika.

Amesema katika kufanya hivyo, suala la Airtel linaweza kushughulikiwa na kupata matunda mazuri zaidi.

Zitto katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii leo Ijumaa Desemba 22,2017 amesema Serikali inaweza kuunda tume kutazama namna ubinafsishaji ulivyofanyika na kuchukua hatua za kisayansi baada ya matokeo ya kazi hiyo.

Amesema akiwa kiongozi wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) walifanyia kazi sera ya ubinafsishaji.

“Katika kila taarifa yetu ya mwaka tulikuwa na sehemu maalumu iliyoeleza ufuatiliaji wetu wa utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji,” amesema.

Zitto amesema ubinafsishaji wa iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni suala walilolitolea taarifa mara kadhaa bungeni na ya mwisho ilikuwa Januari 2015.

“Ni ukweli usio na shaka kuwa kampuni ya Celtel (sasa Airtel) haikulipa chochote kuwezesha kumiliki hisa kwenye Celtel Tanzania na pia uuzwaji wa Celtel kwenda Zain na kisha Airtel ulisababisha Tanzania kupoteza mapato ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax),” amesema.

Hata hivyo, amesema kunahitajika kushughulikia suala la Airtel kwa muktadha wa kazi nzima ya ubinafsishaji nchini.

Zitto amesema PAC iliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi baada ya ubinafsishaji wa mashirika kadhaa, ikiwemo Benki ya NBC na matokeo waliyawasilisha bungeni.

“Uuzwaji wa NBC nao ulikuwa ni wa bure na huwezi kushughulika na kampuni mojamoja bila kutazama muktadha mzima wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma,” amesema.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Serikali ya Magufuli ina miaka miwili madarakani wewe Zito Kabwe tulia wala usiingiwe na kiherehere kwani kama Mungu atamjalia Magufuli na serikali yake kukamilisha miaka mitatu iliyobakia kwa salama basi hata wewe mwenyewe Zito unaweza kushikwa kwa ufisadi. Fagio la Magufuli halitamuacha mtu halitaacha uchafu uwe wa zamani au wa sasa kinachohitajika ni kumpa muheshimiwa raisi na serikali yake ushirikiano wa dhati katika mapambano ya kuijenga Tanzania ya adabu inayoheshimu utawala bora. Utawala bora ni kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaondoa katika hali ya umasikini hayo mengine sijui kuruhusiwa kufanya maandamano au sijui serikali kuruhusu mikutano ya hadhara wachina waliwakanyaga raia wake kwa vifaru baada baadhi ya watu kuamua kuandamana na Dunia ikalaani sana lakini wakuu wa kichina walijua maandamano sio kitu walichokihitaji bali walihitaji mshikamano ili kuijenga China mpya hata wakiutafuta huo mshikamano kwa njia ambazo wengine wasingefurahishwa nazo lakini kwa wao wachina walishikilia msimamo wao na kweli walifanikiwa . Leo unapozungumzia China unazungumzia maendeleo yake maendeleo ya haraka wachina hawakuyapata kwa njia ambazo zito na wenzake wanayahubiri kwa hivyo serikali yetu na Magufuli hawana haja ya kutetereka au kuanza kusikiliza wanaopiga kelele za kuwaondoa malengoni hapana ni kuchukua hatua bila ya uwooga ya kuwaondoa hao wanaojaribu kuikwamisha serikali kufikia malengo yake. Kitu kimoja cha msingi cha kujifunza kutoka kwa wachina ni jinsi walivyo wakali katika kupambana na ufisadi mara nyingi adhabu zake huwa ni kifo. Hapa kwetu mtu kashikwa na ufisadi laivu anapelekwa mahakamani? Nchi inapokuwa corrupted moja katika taasisi zinazoasirika mapema ni mahakama na polisi na bila yakuwa na adhabu kali za mfano kwa wahudumu wa taasisi hizi ni vigumu kushinda vita zidi ya ufisadi.

    ReplyDelete
  2. NSSF NA VIWANJA VYA KIGAMBONI ZITTO INAKUIJIA. KAA CHONJO. NA UJIPANGE VIZURI. MAGU ANAWATU WAKE KOTE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad