Zitto Kabwe azungumzia hatima ya ACT- Wazalenddo


Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe.


Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.


Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha"


Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na jana  Anna Mghwira.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zito amepwerewa.
    anasikitisha.. hiyo play station pia anacheza peke yake.
    Tabia ndiyo iliyomponza.
    wenye akili zao na mwelekeo wote wamesha muhama na hao anaosema madiwani pia qako njiani.
    Anafungua ofisi na ufunguo akiqamaliza kuchaji play station anachwza femu halafu anurudi kutafuta KITECHO FONI CHAKE. Kisa ati na yeye anataka kujismatifonisha.
    ili hali wakati umeshampita. SI USEME kweli zito zuberi kabwe.

    ReplyDelete
  2. Ahaaaa.. Zitto Zuberi Kabwe, Pole mwanagu.
    Loho Inaniumaga nikikuona ulivyo baki Peke yako.

    Sasa nakushauri si ujiungage kule.
    Usione Haya mwanagu.
    Ukweli haujifichi. utabakiaga ukweli Tu.

    Kaombe watakukubali Labda.
    POLE ZITTO MWANANGU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad