Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imemuita naibu balozi wa Marekani mjini Pretoria kufuatia matamshi ya Trump kuhusu nchi za Afrika.
Bwana Trump anaripitiwa kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu wakati wa mahojiano kuhusu sera za uhamiaji.
Amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio mbaguzi.
Taarifa kutoka ofisi ya nchi za kigeni ya Afrika Kusini inasema kuwa inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Muunganoa wa Afrika.
AU ilieezea mshangao wake kutokana na matamsh hayo na kumtaka Trump kuomba msamaha.
Afrika Kusini inasema kuwa uhusiano wake na Mareknia unastahili kuwa katika misingi ya heshima.
Namibia, Botswana na Ghana ni baadhi ya nchi ambazo zimetoa taarifa za kumshutumu vikali Bw. Trump.
Afrika Kusini Yamuita Balozi wa Marekani Kufuatia Matamshi ya Trump Kuhusu Afrika
0
January 15, 2018
Tags