Aibu Kuu: Kilio cha msanii Wastara Bongo Movie Mnatia Aibu

Jana nilibahatika kutazama kipindi kinaitwa Shilawadu, na mwishoni yule mtangazaji akasoma makala iliyoandikwa na Wastara, waraka ule unatia huruma sana na ndani yake unaonyesha kusalitiwa na kutelekezwa mbali na wasanii wenzie wa Bongo movies.

Inaonyesha huyo dada alifiwa na mumewe Sajuki muigizaji, alafu na yeye kwa sasa anaumwa sana na anahitaji msaada kiasi cha kumuangukia Mh. Rais na Makamu wa Rais Mama Samia asipate msaada. Jambo lilinisikitisha ni kukosa msaada kutoka kwa hawa Bongo movies wenzake.

Je? Hakuna chama chao, viongozi wao ambao wanawafuatilia wenzao?
Wasanii wa Bongo Movies amkeni hii Tanzania nyie ndio wasanii na hiyo industry inawahusu ninyi.

 By PastorA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad