Akamatwa kwa Tuhuma za Kujiunganishia Bomba la Mafuta Mali ya TPA Nyumbani Kwake

Akamatwa  kwa Tuhuma za Kujiunganishia Bomba la Mafuta Mali ya TPA Nyumbani Kwake
Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi wanamshikilia Samwel Kilang'ani(63) kwa tuhuma ya kutoboa bomba la mafuta ya dizeli mali ya TPA na  kujiunganishia hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka mantanki makubwa ambayo ameyachimbia chini.

Msemaji wa TPA,  Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.

   
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo kiboko khaa��
    Hii nchi inamchwa wakila aina hatariii. Ushapu wote wa Maghufuli lakini bado watu wanapiga. Kuna watu waliamini Magufuli atashindwa tu kuinyoosha hii nchi ni watu kama hawa na wangali wakimuhisabia Muda labda ndoto zao zitatimia yaani wamekuwa na tamaa ya fiisi aliejisahau na kuingia mjini kwa kuufuata mkono wa binaadamu unaopungwa kwa matarajio labda utadondoka. Mbinu za huyu mwizi si za kimchezo mchezo inataka intelijensia ya hali ya juu kubaini uhalifu wa namna hii. Hongera sana serikali ya awamu ya tano. Watanzania umefika wakati wa kutambua tunapomficha mtu yeyote anaeiibia serikali tusijidanganye yakwamba anaibia serikali na tukapuuzia kama vile hayatuhusu ni ukweli unaouma yakwamba serikali ni sisi watanzania hasa wanyonge na kitendo cha kutomripoti mwizi wa mali za umma ni kitendo cha kuruhusu umasikini ulionao uendelee na kuwacha wachache wakikudhalilisha na kujinata mbeke yako kwa mali zako mwenyewe. Inapaswa kujiuliza kuna mifereji mingapi ya siri ya namna hii?sasa tunafahamu yakwamba kuna mabomaba hewa ya mafuta. Vile vile hapana shaka yeyote kutakuwa yapo ya maji, gas,nakadhalika, hii nchi kiboko.

    ReplyDelete
  2. DA AISEE WATAZANIA NOMA YAAI HUYU JAMAA ALIKUWA KAMA YUKO UARABUNI VILE ANAKISIMA CHA MAFUTA HIVI HATA WATEJA WAKE ALIKUWA ANAWAAMBIA ANAPATA WAPI MAFUTA MAANA NI LAZIMA AYAUZE KIMAGENDO HANA PETROL STATION YAANI WATU WAMEMUHIFAZI MIAKA MINGI SANA WATANZAIA TUBADIRKE TUBAINISHE WATU KAMA HAWA WACHUKULIWE HATUA WAMETUNYONYA SANA MIAKA MINGI

    ReplyDelete
  3. Si huyo tu wapo wengi huko kigamboni

    ReplyDelete
  4. Wezi wanajuana, wambane awataje wenzake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad