Madaktari wameonya kwamba kuzuia kupiga chafya kwa kufunga pua na mdomo kunaweza kukusababishia madhara makubwa.
Hii inajiri baada ya madaktari mjini Leicester kumtibu mtu mwenye umri wa miaka 34 ambaye alipusuka koo kwa kujaribu kujizuia kupiga chafya.
Huku kukiwa hakuna nafasi ya hewa ya chafya hiyo kutoka, ililazimika kupasua tishu laini.
Licha ya kwamba kisa hicho sio cha kawaida, madaktari wameonya kwamba watu wengine wanafaa kujua kuhusu hatari hiyo.
Kuzuia kupiga chafya kunaweza kuharibu masikio mbali na kuathiri ubongo wameonya katika jarida la BMJ.
Mtu huyo anasema kuwa alihisi kuwashwa katika koo yake baada ya chafya hiyo na muda mchache baadaye akaanza kuhisi uchungu na akaanza kushindwa kula na kuzungumza.