Ally Hapi: Waiochukua Hela za Wananchi Ili Wasibomolewe Nyumba Natoa Masaa 72 Wazirudishe

Ally Hapi: Waiochukua Hela za Wananchi Ili Wasibomolewe Nyumba Natoa Masaa 72 Wazirudishe
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi leo January 6, 2018 amefanya ziara Kigogo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na kutoa maagizo kuwa wale wote wanaowadanganya wananchi kwa kuwaambia watoe fedha ili wasibomolewe nyumba zao wazirudishe ndani ya masaa 72 kwani huo ni ulaghai, tulishasitisha zoezi la bomobomoa.

“ Nimetaarifiwa na wananchi wa kigogo kuwa kuna watu wanapitapita kule wanakusanya hela kwa wananchi na baadhi ya watu ni viongozi, sasa nataka niwaambie sina mchezo na kazi yangu, kuna watu wananichezea,”– Ally Hapi

“Wale wote waliokusanya fedha za wananchi na wanaowatisha wananchi kwamba watakuja kubomolewa, wanatumia hicho kigezo kama njia ya kujikusanyia pesa  na baadhi yao ni wenyeviti wa serikali za mitaa, ninawapa masaa 72 wawe wamerudisha fedha zote walizokusanya“– Ally Hapi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad