Aslay Atamani Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph......... Amuomba Amuombee Dua

Aslay Atamani Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph......... Amuomba Amuombee Dua
Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha 'Subalkheri mpenzi' alichoshirikiana na mwanadada Nandy, Aslay amemuomba Mzee Yusuph amuombee dua ili nae siku itakapofika basi arudi katika dini japo kwa sasa hajatizamia hilo.


Aslay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo minong'ono ya chini kwa chini kwamba msanii huyo ameishiwa ubunifu katika kazi zake mpaka kufikia hatua ya kuiga uimbaji wa aliyekuwa muimbaji maarufu wa taarabu Alhaji mzee Yusuph ambae kwa sasa anafanya shughuli zake za kidini.

"Wengi wanafikilia hivyo lakini hata kama nimemuiga Mzee Yusuph sio mbaya maana ukisikiliza 'original' ya wimbo wa Subalkher ni vile vile kama nilivyo imba mimi. Wao walivyokuwa wanaimba ni 'melody' na njia zile zile ambazo sehemu nilizokuwa navuta nawao wanavuta", alisema Aslay.

Pamoja na hayo, Aslay amesema endapo Mzee Yusuph atamsikia basi yeye anamuombea dua katika harakati zake za kila siku.

"Mimi namuombea kwa Mwenyezi Mungu Alhaji Mzee Yusuph anaendeleea na dini na inshallah atuombee na sisi wengine endapo tutakapoona sasa hapa kuna haki ya kumrudia kwenye dini nasi twende. Siwezi sema chochote kwa sasa juu ya hilo suala kwa sababu bado sijajua nini nafanya kutokana na mimi kijana na nina vitu vingi vya kufanya",alisisitiza Aslay.

Kwa upande mwingine, Aslay amewaahidi mashabiki zake hatoweza kuwaangusha katika utendaji kazi wake kwa kuwa hao ndio anawategemea katika kazi zake za muziki.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad