Azam yazipiga Bao Simba, Yanga, Historia Mapinduzi Cup

Ubingwa wa Mapinduzi Cup 2018 ilioutwaa klabu ya Azam, unaifanya klabu hiyo ya Tanzania bara kuandika historia mpya katika mashindano hayo baada ya kuifunga URA kwa penati 4-3 kwenye mchezo wa fainali ulioshuhudia dakika 90 zikikatika huku timu hizo zikiwa hazijafungana.

Azam imekuwa klabu ya kwanza kubeba kombe la mapinduzi mara nyingi kuliko vilabu vyote vilivyowahi kushiriki mashindano hayo tangu yalipoanzishwamiaka 11 iliyopita. Ubingwa wa mapinduzi 2018 ni wa nne kwa Azam ambao waliwahi kutwaa taji hilo katika miaka ya 2012, 2013 na 2017.

Azam wameirudia rekodi yao ya kutetea ubingwa wa Mapinduzi waliyoiweka mwaka 2012 na 2013, mwaka 2012 ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 kushinda kombe hilo ambalo walilitetea tena mwaka 2013. Mwaka 2017 walishinda ubingwa huo kwa mara ya tatu kisha kuutetea tena mwaka huu 2018.

Ukiiondoa Azam, Simba ndio klabu inayofuatia kwa kushinda mara nyingi ubingwa wa Mapinduzi (wameshinda taji hilo mara tatu) katika kipindi cha miaka tofauti.

Msimu huu (2017/18) Azam alipangwa Kundi A pamoaja na URA , Simba, Mwenge na Jamhuri. Katika safari ya kutetea ubingwa wao, Azam walimaliza katika nafasi ya pili wakiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja, URA waliongoza kundi hilo wakiwa na pointi 10.

Mechi za Azam mapinduzi cup 2018 kuanzia hatua ya makundi hadi hadi fainali, Kundi A: Mwenge 0-2 Azam , Azam 4-0 Jamhuri, URA 1-0 Azam, simba 0-1 Azam, Nusu fainali: Azam 1-0 Singida United, Fainali: URA 0-0 Azam (penati 3-4).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad