Baadhi ya Wapinzani Aina ya Lema, Sugu, Lijualikali, Msigwa Badilikeni, ama zimebadilika kwa sasa

Kiukweli awamu ya nne ya Jakaya Kikwete wapinzani mlidekezwa sana ikajengeka baadhi miongoni mwenu tabia ambazo si njema kwa maadili ya kitanzania. Dharau kwa mamlaka, kejeli, matusi, dhihaka na mengineo mengi yenye kuikera jamii ya wastaarbu.

Hili lilichagizwa na kupewa nguvu na baadhi ya vijana waliotumika katika maandamano ya kila mara yasio na tija kwa taifa.

Kipindi cha awamu ya nne ya Jakaya Kikwete baadhi ya wanasiasa wa upinzani walitumia uhuru huo vibaya. Waliposhikiliwa na vyombo vya dola, walitumia makundi ya vijana kuvamia vituo vya polisi kulazimisha waachiwe. Hii kwa waliokua hawajitambui iliwapa kiburi Sana.

Zama zimebadilika kabisa Serikali hii imejikita kurudisha nidhamu iliopote kwa wanasiasa na watumishi wa umma ikijikita kutumikia wananchi ambao upinzani kwa muda mrefu ulituhumu wamepuuzwa.

Kwa sasa vijana na makundi mbalimbali wameelewa dhamira ya dhati ya awamu ya tano katika kuwaondelea kero zilizopigiwa kelele kwa muda mrefu na upinzani.

Kujua hili, hapo nyuma angekamatwa Sugu vijana wa Mbeya wangeandamana aachiwe kwa vurugu nyingi lakini wamemchoka na kumpuuza. Kwa sasa yuko ngomeni na hali ya mji wa Mbeya ni tulivu.

Hali kadhalika kwa Lema, ile miezi minne hatukuona maandamano ya kutaka aachiwe, wamemchoka na kumpuuza. Vijana wako busy wanapambana na shughuli za kujitafutia kipato, wamechoka kutumika pasi na Faida yoyote.

Hili ni funzo kwa wanasiasa model ya watajwa hapo juu.

Wataishia kuilaumu Serikali wakati wao binafsi wanashindwa kutimiza wajibu wao, wanaishi kwa mazoea.

Kikwete aliposema mtamkumbuka mlipomwita dhaifu alimaanisha jambo, sasa mnaona jinsi alivyowadekeza.

Badilikeni, muda bado mnao wa kutosha kwenye uhai wenu, kwani mngali vijana

By thetallest
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hata kitendo cha serikali kupiga marufuku matumizi ya 'VIROBA', pia kumechangia kiasi fulani kuwepo na nidhamu kwa vijana........BIG-UP JPM.....TUMEKUSOMA!!

    ReplyDelete
  2. To be honest kama Magufuli angewaachia hawa wapuuzi wamuendeshe wanavyotaka wao hii nchi ingekuwaje? Nimetumia neno wapuuzi kwa sababu wanaompiga vita Magufuli na jitihada zake za kuinyoosha hii nchi kuja katika misingi ya utu na heshima kwa watanzania wote ili kufikia maendeleo ya kweli ni watu wa kupuuzwa. Kwa kweli haingii hata akilini, mtu au chama kinaweka mikakati ya kivita ya kumtukana na kupambana na Magufuli kwa nia gani hasa? Sera za Magufuli na chama chake zipo wazi kabisa yakwamba nchi yetu tumeibiwa vya kutosha sasa basi. Watanzania tuwache kuzurura hovyo na kupiga domo tukilia kuwa hali ngumu tufanye kazi. Watanzania tulipe na tuzibiti kodi kwani ni ndio uti wa mgongo wa kusaidia kuendesha huduma za nchi yeyote ile duniani. Watanzania rasilimali zetu zilitoroshwa vya kutosha tukiwachwa masikini sasa hali hiyo ikome. Watanzania viongozi wa serikali hata kama angekuwa mke wangu akishikwa na ubadhirifu wa mali ya umma nitamfunga. Watanzania tutapambana kugharamia miradi yetu ya maendeleo wenyewe kwani wenye uwezo hawaoneshi nia ya kutusaidia hata wakionesha nia ya kutusaidia misaada yao ina masharti ya kutudhalilisha. Hizo hapo juu ni baadhi tu za kauli na masisitizo ya muheshimiwa Magufuli. Ni kiongozi alie na un'gamuzi wa mitego kadhaa wa kadhaa ililolipelekea taifa letu kuwa masikini. Tujiulize kwanza? utajiri uliojaa duniani kutoka mataifa na taasisi mbali mbali duniani wakwishindwa kutukopesha katika ujenzi wa reli ya standard gauge tukaweza kuijenga kwa kisu kimoja badala ya kujenga vipande vipande? Ndio maana Africa tumekuwa masikini kwa sababu misaada mingi tunayokopeshwa si misaada amabayo itatuletea ukombozi wa kiuchumi kama huu wa reli ya kisasa unaojengwa Tanzania. Mataifa makubwa mapebari hawataki kuona nchi zetu zikiondokana na hali ya kuwategemea wao na kila mtanzania mwenye akili anapaswa kufahamu hivyo. Haya mataifa mabepari kama yangekuwa na nia ya kweli ya kutunyanyua kiuchumi ni kitu kidogo tu lakini hawana nia hiyo hizo sababu sijui demokrasia sijui blah blah ni upuuzi mtupu kwani kama demokrasi basi nchi za kiarabu zingekuwa za kwanza kuamrishwa kufuata demokrasia lakini ndio washirika wao wakubwa. Mimi nimpe pole Magufuli najua anaumia sana kuona nia yake njema kuna watu au baadhi ya watanzania wakiendesha mikakati ya kopotosha umma ili uendeleze ughasi nchini badala ya kuwa serious na ujenzi wa nchi. Ila tunamuomba muheshimiwa raisi kutovunjika moyo kamwe, kwani kwa uwezo wa Mungu mwenye nguvu zote amewezesha watu wenye nia safi na kujaalia nguvu ya ajabu kwa watanzania tunaokusapoti hadi kuona baadhi ya viongozi wa upinzani wakiachana na hao watu wenye nia chafu na kuungana nawe. Lengo ni kuhakikisha serikali iliyokuwepo madarakani inakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake ya kuwatumikia watanzania na wananchi kwa ufanisi ili kutimiza malengo iliojiwekea. Na jitihada zozote zile za kifisadi zitakazoendeshwa ili kuikwamisha serikali kutimiza majukumu yake ni lazima zipingwe kwa nguvu zetu zote.

    ReplyDelete
  3. Jina au neno la wapinzani NI KUBWA SANA KWA HAWA wahuni. Hawa ni wahuni wa Mitaani na si zaidi ya Hapo.
    Hawajali maendeleo ya wapiga kura wao.
    Kama wangekuwa na Akili Timamu... Si aibu wala haya kumletea maendeleo Mtanzania kwa sababu hutaki kushirikiana na Serikali ya Chama Tawala.
    Sidhani leo mpinzani awe na lake la maana na la kutatua kero ya Mtanzania kwamba wa chama kingine apige hodi kwa Magufuli na aeleze kero za Jimbo lake na asisikizwe na Magu.
    Ila wamejiweka katika mwelekeo na Mikakati ya PINGA KILA KITU na Msishikiane na chama Tawala.
    Magu ameshakuwa ni Raisi wa nchi yetu na ni wa Tanzania yote na Watanzania wote.
    Habagui Dini/Kabila / Rangi/ Chama/ wala huyu wa Mjomba na yule wa shangazi hana Hilo Magu.
    Sasa nyinyi na visakozi nyenu vya kutafuta Ruzuku. Mtaishia hivyo hivyo na mtatumia mbinu na Hila zote za kusema na kutaka kuzihilisha DEMOKLASIA INABANWA. VYUMA VIMEKAZA / SHILINGI IMEKIMBIA.

    usipofanya kazi na usile.... mwisho wake tutakuzika....!!! FANYA KAZI YA HALALI UISHI.

    ReplyDelete
  4. Watanzania jiangalieni sana na Kauli zenu mbaya kwa Wapinzani, ama Mtakuja kuzuavita Tazania.Utawala wa sasa unawaona na kuwato kuwaheshimu, kuwathamini, kuwabana, kuwafungafunga ovyo, na kutowasikiliza. Upinzani umesaidia na bado unasaidia kuwaelimisha na kuwamsha Watanzania kwamba wasilale, wasihujumiwe, maneno matupu hayavunji mfupa, na kuwahusisha katika mambo mengi makuu ya kiuchumi, kujenga sheria sasi na kuzifuata, kujua haki zetu, na kuwakumbusha viongozi wote ya kwamba hayupo aliyejuu ya sheria hata akiwa raisi. Na kitendo cha watu kuabudu watu kama Mungu hakitakiwi. Mtu yeyote mwenye uwezo wa kuishi kufikiri ni haki ya kila mtanzania, Raisi asifikiri kwa niaba ya Watanzania wote, bali awe na uwezo wa kuwasikiliza wananchi mahitaji na matakwa wanayoyapanga, hitaji, na tarajia. Kutokana na haya Raisi kwa kushirikiana na wananchi kwa kufuata sheria ahakikishe matakwa ya wananchi yanatekelezwa vipasavyo.Watanzania hatujawahi kujipangia wenyewe ndio maana wengi wetu hawajui kuwa ni haki zao.
    Tukikubaliana na hili, Watanzania tunaihitaji katiba mpya itakayosimamia na kuhakikisha hayo yote ya juu. Bila Katiba huwezi ukaisafisha nchi ambayo imejiendesha vibaya, imepuuza Wananchi, imeshindwa kutunza, kulinda mali za Watanzania. Yeyote mwerevu, msomi, mzalendo na huenda wako wengi sana. Bila kuubadili mfumo huu, bila kuwachukulia sheria wahusika wakuu waliotuusababishia haya yote, na Maraisi waliopita ndio walikuwa na majukumu makuu na kushindwa kazi. Ni lazima hawa watumbuliwe kwanza, Ni Wapinzani tu tu, ndio wanaoelewa na mara kwa mara wanakazia hili, Tatizo ni chama tawala na uwingi wao, na ndio huko chimbuko la haya yote, MMewahifadhi hawa watu , mnawakingia vifua. Kuna wachache mara mojamoja Bungeni wanasimama na kutaka maraisi wafikishwe mahakamani kutoka CCM, hasa ndugu Bashe. Lakini hajawahi kupigwa, kutekwa, kuweka mahabusu kama wanavyowindwa Wapinzani. Na sifahamu mahakama yetu inafanya nini. Je ni kitengo cha CCM? haki hazitendeki. Nawashangaa sana Watanzania na undumila kuwili, woga, na uongo.Mamilioni ya wasomi bado hawafahamu majukumu yao ya kulikwamua Taifa kupitia elimu. Sasa faida gani ya elimu kama haitumiki vipasavyo. Na wengi waliotufikisha hapa ni wasomi, sababu ya ubinafsi. Ni wazi kwamba elimu hazina faida kwa sasa.Ingekuwa sheria zinafuatwa, na haki zinatendeka, na wezi waadhibiwe vipasavyo, Watu wasingelichezea Taifa letu kama shamba la bibi.Na kwa vile hatujithani, na hatujui thamani zetu, kila mtu anakuja kwa namna zake kuja kutuchezea na kuondoka. Hatuna dume la kusimama kwa majifuno na kujiamini na kujithamini kwa kuweka mikataba. wametoa kama njugu za mtu binafsi. Kosa kubwa kama hili adhabu yake ni kufungo maisha na kutaifisha kila walicho nacho mpaka kwenye mabenki yao ya nje. Lakini Watanzania wapo radhi kwa mwizi wa kuku kupigwa mawe hadharani mpaka kufa, na kumheshu raisi na kumpa kinga na kumpa posho mpaka kufa. Hii inanipa shida kuielewa ni nin Tanzania, Watu wa Tanzania na Sheria za Tanzania zinaruhusu haya. Sasa Mnawaonea bure Wapinzani ambao wanakataa kwa nguvu zote kuunga haya mnawaita Wahuni, Wapuuzi.
    Kama wewe si mjinga afadhali na mpuuzi. Mnamkweza mtu mmoja na hii tumbua si ya usawa, Unatumbua nini na kufuga mapapa. It does not work. Haitafanikiwa kwani hawa watu wameshashikilia uchumi na mamlaka yote. Tusifumbiane macho. Bado naamini kama Ndugu Magufuli ni mzuri, analeta Katiba, na kuwatumbua mapapa. Labda bado anafikiri namna ya kufanya. Na Nampa kazi Bashe aende akamshauri Raisi kwa haya yote kwani anamsikiliza. Hapa nitaisifu CCM.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad