Tupo katika mwezi January, mwezi ambao shule hufunguliwa na wazazi wanakuwa na jukumu la kulipa ada ili watoto waende shule.
Sasa nikusogezee stori kutoka katika eneo la Githurai nchini Kenya ambapo mwanaume mwenye umri wa miaka 39 amejiua baada ya kushindwa kupata ada ya mtoto wake ili aanze kidato cha kwanza.
John Castrol Okombo aliandika ujumbe kabla ya kifo chake akieleza kuwa asingependa kuendelea kuwa hai huku akimuona mtoto wake akishindwa kwenda shule.
Taarifa iliyorushwa katika Television ya Citizen imemnukuu Okombo katika ujumbe huo akisema kwamba asingeweza kuishi na kumuona mtoto wake akishindwa kuendelea na masomo wakati kuna mtu alimtapeli Ksh 759,000 ambayo ni zaidi ya Tshs Milioni 16 za Kitanzania.
Katika ujumbe huo, Okombo ameeleza kuwa mtu aliyemtapeli anaitwa Oliver ambaye hajamlipa pesa zake kwa kipindi cha mwaka sasa.
Okombo alimuagiza Oliver kutuma pesa kwa mke wake ili ziweze kumsomesha mtoto wao pia alimuagiza mke wake kuuza shamba lao ili aweze kumlipia ada mwanafunzi huyo.