Batuli Aitetea Tasnia ya Filamu, Muziki "Inachafuliwa na Wanaojifanaya Wasanii Kumbe Sio Asilimia Kubwa Wanapost Picha Chafu Mitandaoni"

Batuli Aitetea Tasnia ya Filamu, Muziki "Inachafuliwa na Wanaojifanaya Wasanii Kumbe Sio Asilimia Kubwa Wanapost Picha Chafu Mitandaoni"
Msanii wa filamu, Batuli amefunguka kwa kudai kuwa tasnia ya filamu na muziki inachafuliwa na watu ambao wanajifanya wao ni wasanii kumbe sio.

Muigizaji huyo amesema hayo baada ya Naibu Waziri wa Habari,Juliana Shonza kumtaka Gigy Money kuripoti ofisi kwake kutokana na kupiga picha za nusu uchi huku mwanadada Pretty Kind anayedaiwa kuwa ni msanii wa filamu akifungiwa miezi 6 kujihusisha na kazi za sanaa.

“Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu kwenye mitandao hawapo kwenye makundi haya mawili muziki na filamu, umaarufu wao wameupata kwa kupiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii na watanzania wasio na maadili kuwapokea kwa shangwe #SanaaIpeweHeshimaYake,” alisema Batuti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad