Bilionea namba moja kwa utajiri duniani, Bill Gates amemuonya Rais wa Marekani Donald Trump kwa kauli mbiu yake ya "Marekani Kwanza" kuwa inaweza kuharibu uhusiano wake na Afrika.
Bill Gates ametoa kauli hiyo katika mkutano wa dunia wa uchumi Worl Economic Forum unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kunatakiwa kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo na kuanisha kwamba asingependa kuona uwiano huo unapotea.
Bill Gates amesema kwamba Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika kwa nchi kama China ambazo zinazidi kuwekeza barani Afrika, Bill Gates ambaye anamfuko wake unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, umekijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa barani Afrika.
Lakini rais Trump amesema kwamba atakata msaada wa bajeti wa afya kwa takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia. Pia Trump aliwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.