Bodi ya Filamu Wamaliza Beef na Kampuni ya Utaarishaji wa 'Filam Utu Wangu'

Bodi ya Filamu Wamaliza Beef na Kampuni ya Utaarishaji wa 'Filam Utu Wangu'
Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) kupitia kwa Katibu Mtendaji wake Bibi. Joyce Fissoo, wamefanikiwa kumaliza tofauti zilizokuwepo kati ya Sikujua Mbwembe ambaye ni mtayarishaji wa filamu ya ‘Utu Wangu’ dhidi ya Kampuni ya Steps
Entertainment.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Dilesh Solanki
akibadilishani mihutasari ya kikao cha usuluhi wa madai ya msanii wa filamu Sikujua Mbwembwe

Sikujua alikuwa na tofauti na kampuni hiyo ya usambazaji wa filamu kutokana na kuidai fedha zake kutoka kwenye filamu hiyo ambapo kutokana na kikao hiko ameahidiwa kulipwa fedha zake hizo anazodai kuanzia February 5 ya mwaka huu.



Soma barua hiyo hapo chini.

Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.

Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Dilesh Mkurugenzi wa Steps kwa kukubali wito lakini pia kukiri kuwa msanii huyu hajalipwa stahiki zake na kuamua kumaliza suala hili kwa kumlipa kwa jasho lake Bibi. Sikujua” alisema Mama Fissoo.

Mama Fissoo ameishukuru Kampuni ya Steps kwa hatua ilizochukua na kusema kuwa huo ni muendelezo way ale ambayo walikubaliana huko awali ikiwemo kuwalipa wale wote wanaoidai Kampuni hiyo jambo ambalo wameanza kulitekeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki amesema kuwa wao kama kampuni inayojihusisha na mambo mbalimbali ikiwemo usambazaji wa filamu hawafurahishi na kuona wana ingia migogoro na wasanii kwa hao ndio wateja wao muhimu.

Aidha amesema kuwa shida ambayo ilipelekea kutoka kwa tatizo la malipo kwa msanii huyo ni kitendo cha kuwepo kwa mtu wa kati ambaye kwa kiasi kikubwa bndiye amekuwa akifanya mawasiliano nao tofauti na mhusika mkuu.

Kwa upande wake Msanii Sikujua Mbwembwe ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kusema kuwa ameamini kweli kwamba Awamu ya Tani ni Serikali ya kutetea wanyonge ndiyo maana leo hii haki yake anaenda kuipata kwani ameangahika kwa muda mrefu sana.

“Binafsi nipende kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Ofisi yetu ya Bodi ya Filamu Tanzania, nimeleta malalamiko yangu tumekaa vikao vitatu haki yangu imepatikana keli Mungu ni mwema sana” alisema Bi. Sikujua.

Sikujua Mbwembe ni msaani mwenye ulemavu wa miguu ambaye alitayarisha filamu yake ya Utu Wangu na kuingia mkataba na Kampuni ya Steps Entertainment na kukutana na misukosuko katika malipo yake hata hivyo hii inaonyesha alipita katika njia zisizo sahihi, pamoja na yote hayo baada ya kuwasilisha madai yake katika mamlaka husika suala lake limeshughulikiwa na sasa anataraji kulipwa fedha zake na kunufaika na jasho lake mwenyewe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad