Bond Afunguka Kuhusu Kuhusika Kwenye Ujambazi na Kuachana na Wastara

Bond Afunguka Kuhusu Kuhusika Kwenye Ujambazi na Kuachana na Wastara
MENEJA na aliyekuwa mpenzi wa msanii wa Bongo Muvi, Wastara Juma, Bond Suleiman amefunguka kuwa mwaka 2017 ulikuwa ni mchungu sana kwake, baada ya kuhusishwa na tukio la ujambazi na ishu ya kuachana na Wastara.


Wastara Juma akiwa na Bond Suleiman.

Akizungumza na Za Motomoto, Bond alisema kuwa kwenye uhusiano aliumia sana kumuacha Wastara hasa baada ya kumuona ni kama anataka mafanikio ya haraka wakati yeye uchumi ulikuwa umeyumba.


“Mimi ndiye niliyemuacha Wastara na kuamua kuondoka zangu na kwenda kufanya maisha yangu mengine kwa sababu niliona kama namkosesha amani na pia alitaka mafanikio ya haraka wakati uchumi wangu uliyumba. Pia ishu ya kuhusishwa kwenye ujambazi ilinitesa sana kwani nilikaa selo siku ishirini ila nashukuru polisi waliujua ukweli nikawa huru,”alisema Bond.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad