Breaking News: Rais Magufuli Amtumbua Mkurugenzi Butiama

Breaking News: Rais Magufuli Amtumbua Mkurugenzi Butiama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 23, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule kuanzia leo kutokana na ubadhirifu wa fedha za Umma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza maamuzi hayo leo zikiwa zimepita siku tatu toka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Waziri Mkuu aliagiza kiongozi huyo kuchunguzwa kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya Halmashauri hiyo huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazikujulikani zimetumikaje.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahaha watanzania wengi ni wezi sugu ccm imetuingiza kwenye tamaa mbaya na wizi sasa si kila siku boss wao anawaambia wakiiba atawatumbua na wao wanaendelea kuiba sasa inabidi aongeze adhabu unatumbuliwa ama unafilisiwa na kwenda jela ama unaenda jail...........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad