MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu ya gereza la Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya na kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.
“Kosa walilolitenda washtakiwa ni kutoa maneno ya fedheha yanayomtaja rais kuwa muuaji hivyo wakiwa nje wanaweza kupata matatizo kwa wananchi ambao hawajapendezwa na maneno hayo,” alidai Wakili Pande.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana.
Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya ambapo Sugu anadaiwa kutamka kuwa rais ni muuaji.
Tena kabisa , kutukaniwa au kumkejeli laisi wetu... Hilo hatulivumiliiii.
ReplyDeleteMwasweke kwa muda mpaka Hasila zetu zipungue.
hakuna lolote uonevu tuu.
ReplyDeleteEe Tanzania, tunalwenda wapi sasa. Nanyo watu wa ccm mnapoligawa Taifa namna hii na kutokuikosoa serikali kwa jambo kama hili. Mnafikiri ni upinzani tu wanaumia ni nyinyi wanaccm ndio mnaochochea mpasuko wa nchi. Mnapendelewa kama watoto, mnakuwa kama hamfikiri mmeshika dola bila kuhakikisha kila binadamu anatendewa haki. Mnakubali polisi wazuie kila mkutano ya upinzani. Mnakubali wapinzani wanyanyaswe kama di watanzania. Mnakubali watu watekwe na mnatetea hili. Mnakubali mizoga ya watu iokotwe baharini kama si binadamu.mnkubali kutokupeleleza ni nani mhusika wa mambo haya ya kinyama. Mnapata faida gani.wala hakuna mmojawenu anayediriki kuto kuunga mambo ya ki n yama kama haya.watu mamilioni mnaunga mkono huu ubabe, unyanyasaki na mdadiriki kuunga mkono na kumshitaki Lisu kama hamjasoma, hamna uzalendo, hamjali ni kweli maelfu yote ya ccm mnafikra moja.mn
ReplyDelete