Bunduki Zatumiwa Kuunda Hedifoni za Simu

Bunduki Zatumiwa Kuunda Hedifoni za Simu
Kampuni ya Yevo Labs kutoka Sweden imeanza kuunda hedifoni (kisaa cha kutumiwa kwenye simu au kompyuta kusikilizia) ambazo zinaundwa kwa kutumia vyuma kutoka kwa silaha haramu.

Kifaa cha kutia chaji kwenye hedifoni hizo, pamoja na sehemu muhimu ya hedifoni hizo, vimeundwa kwa chuma ambayo imepewa jina Humanium.

Matukio 10 makuu mwongo mmoja wa iPhone
Imeundwa na kundi linalojiita Humanium Metal Initiative, lenye makao yake Sweden, na inatumiwa na kampuni kadha za kutengeneza bidhaa za eneo la Scandinavia.

Mchanganuzi mmoja amesema wazo hilo ni zuri sana na litafanya wanaotumia hedifoni hizo kuonekana wa kipekee, kwani zinapendeza.

Afisa mkuu mtendaji wa Yevo Andreas Vural amekiri kwamba bei yake ya $499 (£370) ni ya juu mno, lakini amesema asilimia 50 ya pesa hizo zitatumwa kwa shirika ambalo hutengeneza na kuuza chuma hiyo.

"Ndicho kitu cha thamani zaidi duniani unachoweza kupata kwa sababu huwezi kukadiria thamani ya uhai wa binadamu," amesema.

Hedifoni hizo ni miongoni mwa vifaa na teknolojia mpya ambazo zimekuwa kwenye maonesho ya teknolojia ya kila mwaka yanayoendelea Nevada.

Bw Vural amesema ilichukua miaka miwili kujua jinsi ya kutumia chuma hiyo kwenye hedifoni.

Shehena ya kwanza ya Humanium ilitoka kwa bunduki haramu zilizotwaliwa na serikali Amerika Kusini.

Hedifoni hizo zinatumia teknolojia ya NFMI (inayotumia nguvu za sumaku) badala ya nyaya, na pia zinatumia teknolojia ya Bluetooth.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad