Tukio la juma Nyoso kumpiga shabiki baada ya mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Simba bado limeendelea kuibua mijadala mbalimbali kitaa, wapo ambao wanamlaumu mchezaji huyo kwa tukio hilo lakini kuna upande ambao unataka kujua kwa nini Nyoso alifikia hatua ya kumpiga shabiki kabla adhabu haijatoka.
Mtangazaji wa Clouds FM Gardner G Habash amesema ni vyema kuangalia kwanza nini kilitokea kabla ya Nyoso kumpiga shabiki kabla ya kuanza kumhukumu.
“Hatusemi alichofanya Nyoso ni sawa, lakini tuangalie kitu gani kilimtokea mpaka akafanya lile kosa kwa sababu alipopewa adhabu mara ya kwanza kama tunanakumbuka alikuwa memfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana kwa Bocco, adhabu aliyopewa haikutokna na mazingira ya uwanjkani au ripoti ya mwamuzi adhabu aliyopewa ilitokana na ushahidi wa video na picha ndio TFF wakaifanyia kazi.”
“Adhabu aliyopewa ilikuwa kubwa hadi watu wakalalamika, kwa sababu alifungiwa kucheza soka kwa miaka miwili. Adhabu ilikuwa kubwa sana afadhali wangempiga faini au wangemwambia asicheze tena mpira kwa sababu hata ukienda kwenye kanuni za FIFA sijui kama kuna adhabu za kuzuia wachezaji kucheza kwa muda huo.”
“Baada ya adhabu ya TFF kutoka ikatoka video nyingine ambayo ilikuwa ndefu kidogo kuliko ile ya kwanza iliyotumika kama ushahidi kwa TFF, video hiyo ilikuwa ikionesha chanzo kwa nini nyoso alifanya tendo lile, alitendewa jambo kwanza likamuudhi kabla ya yeye kulipiza. Alikosea kulipiza na alistahili kuadhibiwa lakini sijui kama adhabu ile ndiyo ilikuwa inamstahili, ilipotoka video ya pili Bocco anaonekana anampiga mateke Nyoso kwa kumchoza mbona TFF haikutoa adhabu?”
“Kwa nini wakati ule Nyoso alikaa kimya hakulalamika? Mimi niliwahi kumtafuta akiwa ameshatumikia adhabu kwa miezi sita nikamwambia kata rufaa labda utasikilizwa akaniambia klabu yangu imenikataza kusema chochote wao wapo kwenye mchakato wanaendelea na masuala hayo lakini hadi miaka miwili ikaisha hakuna mtu aliyemtetea.”
“Miaka miwili baadaye linajitokeza tena jambo kama lile na ninaona kutakuwa na ukimya hakutakuwa na mtu wa kumtetea Nyoso hata angalau kutia shaka kwa nini Nyoso alifanya kitendo kile wengine wanasema yule kijana alimtusi lakini kuna ukimya, jambo la kukamatwa na polisi hatuwezi kulaumu kwa sababu wanafanya kazi yao walimkamata kwa kosa la kumpiga mtu au kupigana hadharani ambapo kwa mujibu wa taratibu za nchi ni kosa.”
Hatakama alifanywa nini, hakutakiwa kuchukua sheria mkononi......ndio maana mwizi akikuibia ukimpiga mpaka akafa, 'jumba-bovu-litakudondokea', tatizo ni KUCHUKUA-SHERIA-MKONONI
ReplyDelete