CHADEMA Iringa yapata pigo tena.....Madiwani Wawili Watimkia CCM

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili kutangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wakiongea na waandishi wa habari aliyekuwa diwani wa Ruaha, Tandesy Sanga ambaye ametangaza uamuzi wa kujiuzulu jana  Jumatano Januari 3, 2018 jijini Dar es Salaam na mwenzake wa Kwakilosa, Joseph Ryata ambaye yeye aliandika barua ya kujiuzulu toka Disemba 2017 na kusema kuwa wamefanya maamuzi hayo kutokana na mgongano wa maslahi ndani ya CHADEMA.

Joseph Ryata amedai kuwa wao uamuzi wao wa kwenda Chama Cha Mapinduzi upo tofauti na wale wengine ambao wanadaiwa kununuliwa na baadhi ya viongozi wa CCM

"Mnamo Disemba 22, 2017 nilifanya maamuzi mwenyewe wala sikushinikizwa na mtu niliamua kujiuzulu nafasi ya udiwani wa Kata ya Kwakilosa na nilifanya hivyo kwa sababu za msingi zifuatazo sikuwa na ushirikiano mzuri na wenzangu.

"Kumekuwa na wimbo la madiwani kuhama lakini niwahakikishie kwamba kuhama kwangu mimi hakuendani na hilo wimbo ambalo linazungumzwa kwamba madiwani wananunuliwa wanahama bali kuhama kwangu mimi ni migongano, kutokuelewana, na kule kutofuata mifumo ya kichama ya uendeshaji mzima wa baraza la halmashauri ya Iringa Mjini" alisema  Ryata

Mbali na hilo Ryata amesema kuwa uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Manispa ya Iringa Mjini haukufuata utaratibu na kudai kuwa ulitumika ubabe na mabavu kuendesha zoezi hilo ambalo kila baada ya mwaka linapaswa kufanyika illi kuwapata viongozi wapya wa baraza.

Mpaka sasa Manispaa ya Iringa Mjini imepoteza madiwani wa Kata sita ambao wote baada ya kujiuzulu walijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad