Chadema Wakanusha Taarifa za Kuugua Ghafla Katibu Mkuu Wao

Chadema Wakanusha Taarifa za Kuugua Ghafla Katibu Mkuu Wao
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, DR.Vincent Mashinji amelazwa katika hospitali ya Amana baada ya kuumwa ghafla.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA bwana John Mrema amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kudai kuwa Katibu wao ni mzima wa afya na sasa anaendelea na kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kinachofanyika Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

"Tumeiona hiyo taarifa ila si ya kweli na sijui wameitoa wapi kwani Katibu Mkuu ni mzima wa afya njema na hivi naongea na wewe tupo naye kwenye vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA hapa Bahari Beach" alisema Mrema

Mapema leo zimezuka taarifa kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA ameugua ghafla na kupelekwa hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi na kuwa alitembelewa na Katibu Mkuu wa CUF akiwa hospitali hapo, japo ambalo limepingwa  na Bwana Mrema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad