Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.
Mbowe ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.
“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”
Hiyo kauli ya Mbowe ya kuhimiza udini katika siasa ni kitendo cha hatari na kipumbavu kabisa. Kule Zanzibar kulikuwa na kikundi cha Dini cha Mwamsho ni kikundi kilichokuwa kinaongozwa na Masheikh waliokuwa wakihubiri siasa na inasemekana Masheikh wale walikuwa wakisapotiwa na baadhi ya vyama na viongozi wa upinzani. Kikundi kile cha mwamsho kiliendesha mahubiri yake ndani ya nyumba za ibada na walipopata nafasi walihubiri katika mikutano ya hadhara. Waliwahubiria wazanzibari kuichukia serikali yao kwakuwa haikuwa ikiwatendea haki hasa kwa kuwaruhusu watu wa upande wa pili wa Muungano kuimiliki Zanzibar . Baadhi ya biashara za watanzania na Makanisa yalitiwa moto baada ya hisia kali na za chuki kujaa kwa wafuasi wao. Baadhi ya watu na viongozi wa dini waliokuwa na misimamo tofauti na mwamsho walimwagiwa acid au tindi kali kuna waliofariki na wengine mpaka leo ni vilema . Mbowe na wenzake wanaelekea sio tu kuishia kuwahimiza viongozi wa dini kuhibiria siasa makinisani bali viongozi wa dini wengi wamefungamana na makibila yao na wanamvuto mkubwa sana katika makibila yao na wengi wao wana heshima ya uongozi wa kabila analotoka kwa hivyo uwezekano wa kuleta mvutano wa makibila na kuleta mvurugano wa umoja wa kitaifa ni mkubwa. Kuukweli huwezi kumuelewa Mbowe kwa kitendo chake cha kuwahimiza viongozi wa dini kuanza kuwahubiria waumini wao siasa? Unaweza kusema ni maarifa ya kisiasa alieyaazima kutoka kwa Cuf maalim seif kule Zanzibar. Kule Uganda kuna kiongozi wa dini aneongoza kikundi cha ughasi anaeishi msituni alianzia kama kakobe tu. Kiongozi wa imani ya dini fulani
ReplyDeleteakianza kuikosoa serikali hapo hapo akatokezea kiongozi mwengine wa dini mwenye imani tofauti na kuanza kupingana nae haiwezi kuwa ndio chanzo cha mvutano wa kidini? Mara kadhaa viongozi wa upinzani wameonyesha hamu ya kutaka amani ya nchi inapotea kwa kisingizio cha kuikosoa serikali. Na kama Mbowe anamawazo ya njia ya mkato zaidi kukijenga chama chake kwa kupitia siasa za makinasani sisi tunasema hiyo ni tamaa ya hatari zaidi kwa amani ya nchi ni sawa na kuendesha gari ukiwa umelewa katika ya mlima wa kitonga kwa tamaa ya kufika haraka. Ni ukosefu wa tafakari makini kuruhusu makundi ya dini Katika Taifa ambalo linamchanyiko wa imani tofauti za dini kuhubiri siasa. Ikiwa mwalimu Nyerere alisema kiongozi mwenye tamaa ya hubiria udini ili kujijenga kisiasa ni mtu wa kuogopwa kama ukoma nitashangaa sana kuona watanzania wakikaa kimya bila ya kulaani kauli na tamaa ya Mbowe kwani ina nia ya kulitumbukiza taifa katika machafuko na kupelekea umagikaji wa damu.