Dereva Alivyookoa Abiria Katika Basi la Tahmeed Lililowaka Moto


Basi la Kampuni Ya Tahmeed lenye namba za usajili T483 BFL limeungua moto katika Kijiji cha Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga leo Januari 29, 2018.

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, SACP Edward Bukombe, basi hilo ambalo lilikuwa na abiria 9 likitokea jijini Dar es salam liliungua moto kutokana na hitilafu za umeme wa gari.

Alisema Dereva wa basi hilo, Bakari Said (34) alihisi halipo vizuri katika mfumo wa injini ndipo akasimamisha gari kisha kuwaomba abiria wote watoke ndani ya basi.

Kufuatia hatua hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo. Hii ni mara ya pili kwa basi la kampuni hiyo kupata hitilafu kwenye mfumo wa injini na kuungua moto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad