Dkt Shein Ataka Ofisi ya Takiwimu Kuandaa Sera ya Kusimamia Ukusanyaji wa Takwimu

Dkt Shein Ataka Ofisi ya Takiwimu  Kuandaa Sera ya Kusimamia Ukusanyaji wa Takwimu
Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein amesema ipo haja kwa ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali kuandaa sera ambayo itatoa muongozo wa kusimamia ukusanyaji wa takwimu kwa Tanzania Bara na visiwani.

Rais Shein ameyasema hayo wakati wa ufunguzi Jengo la Mtakimu Mkuu wa Serekali Mazizini Zanzibar, ambapo pamoja na hayo aliomba Mawaziri kushirikiana.

“Lazima tuandae policy ya statistics, tumebahatika tu kwa matatizo yaliyokuwepo tukatunga sheria kwanza, lakini ustaarabu wa suku hizi unatengeneza sera kwanza halafu unatengeneza sheria halafu kanuni sisi tulifanya kinyume kutokana na haja tuliyoifanya bado tunahitaji kutengeneza sera ya Takwimu,” alisema Dk. Shein.

Hata hivyo Dkt Shein aliwaagiza Mawaziri wanahusika na mambo ya Muungano kushirikiana katika mbalimbali kwa faida za pambe zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad