DPP Awapa Maagizo Takukuru Kuhusu Jarada la Kesi ya Malinzi

DPP Awapa Maagizo Takukuru Kuhusu Jarada la Kesi ya Malinzi
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewarejeshea TAKUKURU jalada la kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake ili warekebishe vitu vichache vya kiuchunguzi.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Hayo yameelezwa na Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai amedai jalada la kesi hiyo limesharudi TAKUKURU likitokea kwa DPP, hivyo wamepewa maelekezo ya kukamilisha baadhi ya uchunguzi.

Baada kueleza hayo, wakili wa Utetezi Nehemia Nkonko aliomba upelelezi wa shauri hilo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad