Familia Yajipanga kumpa Taarifa Kiingune Juu kifo cha Mkewe

Familia Yajipanga  kumpa Taarifa  Kiingune Juu kifo cha Mkewe
Familia ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru imesema inasubiri baba yao apewe taarifa za msiba ili wajue taratibu za mazishi za mkewe Pares Mwiru.

Akizungumza na Mwananchi  leo Ijumaa Januari 5, 2017 nyumbani kwa Kingunge, mtoto wake Tonii Ngombale amesema baba yao hadi sasa  bado hajapewa taarifa ya kifo cha mkewe.

Amesema hali hiyo imetokana baba yao kuwa bado yupo  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na mbwa.

"Taratibu  za mazishi zitafahamika baada ya mzee (Kingunge), kupewa taarifa .Tunamsubiri atoe kauli kwa sababu yeye ndio mwenye mji wake na kiongozi  wa familia," amesema  Tonii na kuongeza kuwa

"Hatuwezi kufanya jambo lolote kwa sasa bila yeye kutoa kauli. Tunasikitika kumpoteza mama yetu, lakini wakati huo huo tunaomba dua hawezi kupokea taarifa hii  ya msiba katika hali  nzuri," amesema Tonii.


Tonii amesema jioni wazee wenzake  watajipanga na kwenda hospitalini kwa ajili ya kumpa taarifa za msiba wa mkewe kisha watatangaza utaratibu  wa mazishi hayo.

Pares Mwiru  alifariki dunia jana Alhamisi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad