Hatimaye Rugemalira Awataja Wezi wa Fedha za Escrow Mbele ya Mahakama

Hatimaye Rugemalira Awataj Wezi wa Fedha za Escrow Mbele ya Mahakama
MFANYABIASHARA, James Rugemalira anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja aliodai ni wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyosema awali kwamba anawafahamu.

Watu hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,  baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Ruswa (Takukuru), Leonard Swai,  kueleza kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 Baada ya kuelezwa hayo, wakili wa utetezi, Michael Ngalo, ameomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi hiyo na kama hawawezi waiondoe mahakamani.

 Baada ya kuelezwa hayo, Rugemaliraa alinyoosha mkono ambapo alidai yeye ni mgonjwa wa kansa kwa miaka tisa sasa na amekuwa akipatiwa matibabu nchini India, lakini kwa sasa ugonjwa huo umejitokeza kwa njia ya uvimbe katika sehemu za siri.

 Akiiambia mahakama kuhusu suala la aliodai ni wezi, Rugemalira alidai alishawasilisha nyaraka za ushahidi kwa Takukuru kwamba ‘mwizi’ aliyeisababishia serikali hasara ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao waliisababishia  hasara ya Sh. trilioni 37.

Pia amedai kuwa watu hao aliowaita wezi hao ndiyo wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Sh. trilioni 16.

 Naye mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi, aliiambia mahakama hiyo kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana, pia yupo tayari kutoa ushirikiano wowote zikiwemo nyaraka ili kubaini ukweli wa kesi hiyo.

Baada ya kueleza hayo, wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemalira aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Akitoa ufafanuzi, Hakimu Simba alisema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia ameutaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watajeni hawa vigogo. Mnawaficha kwa nini. Kuna mawazri na mawakala kupitia Ikulu wengi tu. Mtu wa kawaida hawezi kufanya jambo kubwa kama hili bila mkuu kuhidhinisha. Ni hao ambao walitetea na kukanusha wazi pesa si mali za umma au Watanzania. Wote walijua hili. Watu mnaogopaje kuwataja hawa. Na ni hao waliidhinisha mengi sana na mikataba mikuu yote. Angalieni safari za nje Alikuwa Raisi na wengi wenu. Hili kundi lote linajulikana wazi. Sasa mnasema mmempata kiboko anaye tumbua lakini mnawakingia kifua hawa watu kuna Maraisi na mawaziri na kundi zima liko CCM. Ilikuwa ni rahisi kumtaja Huyu mama wa Kagera aliyepewa kipesa cha mboga mkamweka chambo tu. Nyinyi wenyewe madume mnashindwa kujitaja sababu mikono ya watu hawa ni michafu sehemu nyingi tu. Lakini hata wakifanyaje, Watatolewa tu hadharani. Wamempa maneno mazuri Kafulila ili aache speed sijui ni donge gani kapewa kuuza utashi na uhodari wake wote. Wanajua kule watamzatiti. Elimu yote kaiweka kando. Kamsahau hata mkewe ambaye alisimama nyuma yake twenty four hours. Mwanamke kagoma. Utu na uzalendo wa Watanzania ni homa. Labda alipokwenda marekani na kule kulikuwa na baadhi ya watu wa Standard bank wamempa jeki fulani asiendelee tena.
    Aibu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad