"Hii ni Dunia Nyingine"- Papii Kocha

"Hii ni Dunia Nyingine"- Papii Kocha
Mtoto wa msanii nguli wa muziki wa dance, Papii Kocha amefunguka na kudai maisha ya uraiani ni sawa na dunia nyingine kwani mtu akiwa anatumikia adhabu ya kifungo gerezani, huwa vitu vingi vizuri anashindwa kufanya ama hata kushiriki kabisa.

Papii ameeleza hayo pindi alipokuwa kwenye matayarisho ya ujio wake mpya katika muziki akiwa pamoja na Baba yake Nguza Viking maarufu kama Babu Seya ambapo wawili hao walitoka jela kwa msamaha wa Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru yaliyofanyikia katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma mwaka huu.

"Miaka 14 siyo mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliya-miss, nime-miss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine", alisema Papii Kocha.

Pamoja na hayo, Papii ametoa ahadi kwa mashabiki na wapenzi wa 'dance' kwa kuwapa kitu kilichokuwa bora zaidi tofauti na zile walizokuwa wamezifanya kipindi cha awali.

"Tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad