Dkt. Shika amekiambia kituo cha runinga cha Azam kuwa anachoshughulikia kwa sasa hapa nchini ni kuingiza fedha zake zilizopo nje ya nchi ili awe kufungua kampuni na itakapoanza kufanya kazi ndipo atasafiri.
“Basi nitakuwa nimemaliza kazi yangu kwa hapa Tanzania ninaondoka kwenda Marekani kuitumikia dunia, mimi ni balozi katika Umoja wa Mataifa uteuzi ambao ulifanywa 2014 na sikuripoti kazini lakini hawajakata tamaa miezi miwili iliyopita nimepandishwa cheo kwa ngazi ya juu,” amesema Dkt. Shika.
“Mwanzo niliteuliwa kuwa balozi wa wakimbizi kwa upande wa Afrika, sasa nimechaguliwa kuwa balozi wa wakimbizi ulimwenguni kote, kwa hiyo ofisi kutoka Nairobi inahama kwenda New York,” amesisitiza.
Utakumbuka umaarufu wa Dkt. Shika ulikuja baada ya kujitokeza katika mnada wa kuuza nyumba za Lugumi ambapo aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800, kisha kudai anangojea fedha zake kutoka nchini Urusi.
Unatisha Dokta Shika.
ReplyDeleteUsimsahau Meneja wako Catty Kahabi
Kila la heri, usisahau TZ ndo home
ReplyDeleteDkt Shika..!!!
ReplyDeleteUnazidi kutisha....!!!
Sasa zile za kutoka Tailandi vipi?
Na nyumba zako utamwacha nani kuzisimamia?
Nie niko tayari kuziangalia na kuku kusanyia Kodi ila ujue kodi ya selikali ntakulipia kutoka kodi za nyumba.
Sasa PPt yako wamekupa langi gani?
Ya kidiplomati au ile ya Misheni...?
Mie lazima nikutafute Dkt... Sema unawapambe wengi hata selfi sikuweza kuipata.
Lakini sivunji tamaa... Ntakuona tuuu.