"Huyu ndiye Tundu Lissu Mdogo" - Kubenea

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.


Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha, Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini ambao wanapaswa kufika Bungeni kuwatetea wananchi wa Kinondoni.

"Nina mfahamu Salum Mwalimu ni kati ya waandishi wa habari wachache nchi hii walio jasiri na wasioogopa wanafanya kile wanachokiamini, ameandika stori kubwa na kuripoti matokeo makubwa sana na kutetea hazi za binadamu, amefanya kazi kubwa kutetea misingi ya uandishi wa habari mkimpeleka Bungeni mtakuwa mmetupeleka chachu nyingine, mtakua mmemleta Lissu mwingine mdogo na kwenda kumpandikiza Bungeni" alisema Kubenea 

Mbali na hilo Kubenea aliwataka wananchi kupuuza maneno yanasosambazwa kuwa Salum Mwalimu si Mtanzania na kusema huyo ni raia wa Tanzania na amekulia Tanzania bara hivyo waachane na maneno hayo yanayosambazwa na watu wa Chama Cha Mapinduzi.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo Kubenea... Umekosa la kusema na Kumuuza Mgombea Wenu na Kumlinganisha au kumfananisha na Kusabilishia Ulingano na Mgonjwa Lizu.
    Je hauoni kama umeshafanya Blander katika kumnadi na Jinsi Watanzania alivyo mjua Lizu katika masuala ya Kupinga maendeleo ya nchi yetu. Wamesha mchoka na sera zake za vuta huku na mimi nivute kele TUKATE KAMBA.
    KUBENEA UMEFANYA KOSA LISILO TENGEMAA NA KATIKA KULA 100 UMEFAZIFANYA ZENU KUWA SI ASILIMIA 2+3 LABDA ZA WALEVI ... LAKINI ZI ULISIKIA VIROBA MARUFU...KWA HIYO ZA WALEVI PIA MTAAMBULIA PATUPU.
    POLENI SANA...WEWE NI WA WAPI PIA...???

    ReplyDelete
  2. Hivyo Kubenea... Umekosa la kusema na Kumuuza Mgombea Wenu na Kumlinganisha au kumfananisha na Kusabilishia Ulingano na Mgonjwa Lizu.
    Je hauoni kama umeshafanya Blander katika kumnadi na Jinsi Watanzania alivyo mjua Lizu katika masuala ya Kupinga maendeleo ya nchi yetu. Wamesha mchoka na sera zake za vuta huku na mimi nivute kele TUKATE KAMBA.
    KUBENEA UMEFANYA KOSA LISILO TENGEMAA NA KATIKA KULA 100 UMEFAZIFANYA ZENU KUWA SI ASILIMIA 2+3 LABDA ZA WALEVI ... LAKINI ZI ULISIKIA VIROBA MARUFU...KWA HIYO ZA WALEVI PIA MTAAMBULIA PATUPU.
    POLENI SANA...WEWE NI WA WAPI PIA...???

    MIE NAKUULIZA MH KUBENEA KAMA LIS MKUBWA HATUKUMTAKA ..JE KUNA UWZEKANO TUKABOTEA MABOYA NA KUMTAKA MDOGO...!!!?? AMBAE AMESHAKUWA CHACHU NA ANA MNUKO TAYARI..????

    JAMANI MJIPANGE KATIKA KUZUNGUMZA NA WATANZANI WA KARNE HII. SI WALE WA KARNE ILE YA MADONGO POLOMOKA!!! MUULIZE
    WSTER NA HALIMA IKIBIDI ZITO PIA?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad