KUNA aina ya vitunguu vinavyotumika katika mapishi, imegunduliwa ina uwezo wa kutibu kifua kikuu (TB) na zingine za aina mbalimbali, utafiti mpya umebaini.
Watafiti wamebaini pia, vimelea na yaliyomo katika vitunguu hivyo, inaweza kuzalisha antibaiotiki inayomudu usugu huo, ingawaje kunahitajika utafiti zaidi.
Aina hiyo ya TB sugu inatajwa takwimu zake mathlan kwa mwaka 2016 pekee yake, iliathiri jumla ya watu 490,000 nchini Uingereza.
Hadi sasa, utafiti huo unaendelea chini ya uratibu wa Chuo Kikuu cha London, Uingereza ulifuatilia kwa kina matumizi wa vitunguu hivyo katika mapishi mbalimbali.
Utafiti umefanywa kwa mara nne tofauti na matokeo ya ripoti zote tofauti, zinaonyesha matokeo chanya, baadhi yakiwa kwa kiwango cha juu asilimia 99.9.
Maoni hayo ya kitaalamu yanaeleza kwamba, tiba hiyo ya kitunguu inaweza kutumiwa sambamba na ile ya kila siku.
Mshiriki katika utafiti huo, Dk. Sanjib Bhakta, ana lake la kuchangia:"Licha ya juhudi za serikali kuzuia kuenea kwa kifua kikuu, ni takriban wagonjwa wapya milioni 10 walipatikana (duniani) katika mwaka 2016.”
Mwanazuoni mwingine, Profesa Simon Gibbons, anasema: "Mazao ya asili na mimea, ina nafasi yake kubwa kama antinbaiotiki. Mazingira ni mkemia mbunifu.”
Anasema mimea hiyo ya asili inazalisha kemikali dhidi ya vijidudu na mazingira.
Mnamo Oktoba Mosi, Mganga Mkuu wa Serikali ya Uingereza, Profesa Dame Davies, alisisitiza kuwa viongozi mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele kupiga vita usugu wa vijidudu dhidi ya dawa za antibaotiki dhidi yao.
Wataalamu wa tiba wanasema kuwa, dawa hizo zinazotajwa kuwa sugu, zinatumiwa na watu wasiopungua 25,000 barani Ulaya, huku Afrika mataifa na shirika yasiyo ya kiserikali na ndio maana wanahisi ugunduzi huo mpya ni hatua inayojitegemea ya mafanikio.