Johari Ana Kidonda Kisichopona

MWIGIZAJI wa kitambo Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa tangu ampoteze mama yake mzazi, Asha Chagula aliyefariki dunia wiki iliyopita, amepata kidonda kikubwa ambacho hakiwezi kupona katika maisha yake yote.


Huku akiwa na majonzi, Johari aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mama yake huyo alikuwa ni nguzo muhimu katika maisha yake kwani alikuwa ndiye mshauri wake mkubwa.

 “Mama yangu alikuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu na amenipa kidonda kikubwa sana katika maisha yangu ambacho hakiwezi kupona milele, ninaumia mno na sijui nitawezeje bila mama yangu,” alisema Johari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad